Vortex Stay Blind Booking

Chagua chumba.Ona bei halisi.

Chagua aina ya chumba na umbali. VortexStay inakuonyesha bei halisi za vyumba vilivyo wazi, kisha inakutafutia chumba. Hulipi hadi hoteli ikubali ombi lako.

Android · Tanzania

  • Bure kupakua
  • Hoteli zimehakikiwa na VortexStay
  • Hulipi hadi hoteli ikubali
Ukurasa wa mbele wa app ya VortexStay
Orodha ya bei halisi
App ikitafuta vyumba vilivyo wazi

Jinsi inavyofanya kazi

  1. 1

    Chagua chumba na umbali

    Aina ya chumba, tarehe, wageni na umbali unaoweza kwenda.

    Ukurasa wa mbele wa app ya VortexStay
  2. 2

    Tunatafuta vyumba vilivyo wazi

    VortexStay inaangalia vyumba vilivyopo kweli karibu nawe, kwa wakati halisi.

    App ikitafuta vyumba vilivyo wazi
  3. 3

    Chagua bei halisi

    Unaona bei za vyumba vilivyo wazi, bila majina ya hoteli. Chagua unayoweza, nasi tunakutafutia chumba.

    Orodha ya bei halisi
  4. 4

    Hoteli ikikubali, unalipa

    Hulipi hadi hoteli ikubali ombi lako. Ikikubali, jina na eneo la hoteli vinafunuliwa.

Kwa nini VortexStay

Bei halisi, bila majina ya hoteli

Unaona bei za vyumba vinavyopatikana kweli, si bei za jina la chapa.

Hulipi hadi hoteli ikubali

Hakuna malipo kwa kutafuta. Unalipa baada ya hoteli kukubali ombi lako.

Hoteli zimehakikiwa

Kila hoteli inahakikiwa na VortexStay kabla ya kuanza kupokea wageni.

Hoteli inapata ombi papo hapo

Ombi lako linafika kwa hoteli mara moja, kwa hiyo unajibiwa haraka.

Kwa wamiliki wa hoteli

Pokea wageni wapya kupitia simu yako. Unasajili hoteli yako mara moja, VortexStay inaihakiki, kisha inakuunganisha.

  • Maombi ya wageni yanakufikia papo hapo kwenye simu yako.
  • Unatumia token kwa mgeni aliyethibitishwa tu, na token inarudi booking ikighairiwa.
  • Hoteli inayojibu haraka inapata wageni zaidi. Hoteli isiyojibu inajipunguzia nafasi ya kupokea wateja zaidi.
  • Hoteli yako inahakikiwa na VortexStay, na unaonekana kama hoteli iliyothibitishwa.

Unachohitaji kusajili

  • Namba ya usajili (Hotel Reg No.) kutoka VortexStay
  • Hati ya usajili wa hoteli (PDF, JPG au PNG)
  • Simu ya meneja, itapokea code ya SMS
  • Uwe ndani ya hoteli, ili eneo lake lithibitishwe

Hatua za usajili

  1. 1Taarifa za hoteli
  2. 2Meneja, thibitisha simu kwa code ya SMS
  3. 3Eneo la hoteli
  4. 4Pakia hati ya usajili
  5. 5Hakiki na utume

Kuwa wakala wa VortexStay

Wakala anasajili hoteli kwenye VortexStay kwa kutumia VORTEX ID yake. Kila wakala anapewa utaratibu na VortexStay.

Wasiliana na VortexStay kwanza. Baada ya hapo utapewa utaratibu wa kujiunga.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

VortexStay ni nini?

Ni app ya kupata chumba Tanzania. Unachagua aina ya chumba na umbali, unaona bei halisi za vyumba vilivyo wazi, na VortexStay inakutafutia chumba.

Kwa nini sioni majina ya hoteli?

Hii ni "blind booking": unachagua bei, na jina na eneo la hoteli vinafunuliwa hoteli ikikubali ombi lako.

Ninalipa lini?

Unalipa baada ya hoteli kukubali ombi lako, ndani ya dakika 10. Kutafuta hakuna gharama.

Hoteli ikikataa au isipojibu?

Hulipi chochote, na unaweza kutafuta tena mara moja.

Nikighairi nini kinatokea?

Hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yako. Ukihitaji msaada kuhusu malipo uliyokwisha fanya, wasiliana nasi kwa WhatsApp.

Naipata wapi app, na kuna ya iPhone?

App ya wateja iko Google Play, kwa simu za Android, Tanzania. Kwa sasa hakuna toleo la iPhone.

Nawezaje kusajili hoteli yangu?

Unahitaji namba ya usajili (Hotel Reg No.) kutoka VortexStay. Ukiwa nayo, jaza fomu ya usajili hatua 5. VortexStay inahakiki hoteli yako, kisha inakuunganisha.

Token ya hoteli ni nini?

Hoteli inanunua token. Token moja inatumika kwa mgeni aliyethibitishwa (aliyelipa au kufika), na inarudi booking ikighairiwa. Kutafutwa hakukati token.

Hoteli yangu isipojibu maombi?

Hoteli isiyojibu inajipunguzia nafasi ya kupokea wateja zaidi. Jibu maombi haraka ili upate wageni zaidi.

Nawezaje kuwa wakala?

Wasiliana na VortexStay kwanza. Baada ya hapo utapewa utaratibu wa kujiunga.

Hukupata jibu? Tuandikie WhatsApp.